Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano
Bwana alimpa Yehu thawabu kwa kutekeleza maagizo yaliyohusiana na nyumba ya Ahabu. LakiniYehu hakuangalia, aende katika sheria ya Bwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote; hakutoka katika makosa ya Yeroboamu, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli(m.31).Yehu hakuwa mwangalifu kuhusu alivyomtumikia Bwana. Utendaji dhambi wa Yeroboamu, mfalme wa kwanza wa Ufalme wa Israeli, ulipata kuendelea. Basi Mungualianza kupunguza Israeli(m.32). Ni sababu halisi ya sehemu kadhaa za nchi kuchukuliwa na kuwa chini ya utawala wa mataifa mengine. Mpendwa, ukiruhusu dhambi fulani iendelee katika maisha yako, unapinga uwepo wa Mungu kwako. Zingatia ilivyoandikwa katika Rum 2:3-4:Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz