Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 1 YA 31

Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

William Booth, Mwanzilishi wa Jeshi la Wokovu, alitoa ujumbe huu wa mwisho tarehe 9 Mei 1912 wenye hayo maneno mazito: ‘Wanawake wakiendelea kulia, kama wanavyolia sasa, Nitapigana, watoto wadogo wakishinda na njaa, kama wanavyoshinda sasa, Nitapigana, …akiwepo msichana masikini aliyepotea mtaani, pakibakia nafsi moja yenye giza isiyo na mwanga wa Mungu, Nitapigana – Nitapigana mpaka mwisho!’

Ahadi ya Booth ya

kupigana bado imesimama katika utume na kazi ya huduma leo. Kwa wengi, mapambano ya kutafuta haki ni ya kweli leo kama yalivyowahi kuwa. Siku baada ya siku mamilioni wanajitahidi kushinda ulevi, unyanyasaji, njaa, upweke, umasikini na mengi mengine. Tuna nafasi na wajibu wa namna gani, kusimama mstari wa mbele na wale ambao sauti zao zinahitajika kusikilizwa, na tupambane pamoja na kwa ajili yao.

Tumaini letu ni kwamba tafakari hizi zitachemsha ndani yako hamu ya ndani ‘ufanye jambo fulani!’.

Waebrania 13:16 inatukumbusha sisi: ‘Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana, maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.’

Changamoto: Mkague jirani au rafiki. Wengi katika jamii zetu wanahitaji msaada wa ziada. Hauwezi kufahamu maswala wanayokabiliana nayo bila kuwaendea na kuwauliza. Kuna jambo jepesi unaloweza kulifanya kumsaidia mtu leo?

Maombi: Mungu, tusaidie tutumie karama na uwezo wetu kuwasaidia wale walio katika jamii zetu walio katika mazingira hatarishi kabisa. Mungu tusaidie kufanya kazi ya kupata haki ndani ya majirani zetu, kwa wanaokandamizwa na wale wanaoumia. Tusaidie kwa neema yako kutii neno lako kila siku na tufanye jambo fulani. Amina.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org