Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 2 YA 31

Kama mwanamke na ‘asiye msafi’, mwanamke huyu bado alithubutu kuja kwa Yesu akiwa na matarajio ya kupata uponyaji. Naye alifanya hivyo. Akapata uponyaji wa mwili na wa roho.

Licha ya kugundua kwake, hata hivyo, alijisikia kuwa na aibu kugunduliwa na jamii, kwani hali yake ilimtenga na maisha ya watu wengi. Kifungu hiki kinatukumbusha kwamba hayupo anayeweza kuwa mbali sana na Mungu asiponywe. Acha tukiri dhambi zetu kwake na tusiyafunike maovu yetu, tutubu dhambi zetu kwake Bwana kwasababu yeye husamehe uovu wa dhambi zetu. (Zaburi 32:5).

Hebu tukumbuke vile vile kwamba haijalishi nani anatuona kuwa hatuna faida na ni wasio na thamani, Yesu anatuona kuwa wenye thamani kuwa mabinti zake, wanaopata uhuru na ukamilifu ndani yake. Licha ya jinsi dunia inavyofanya kazi, jinsi watu wanavyotengwa mara kwa mara kwa sababu ya tofauti zao, naweza kushuhudia kwamba bado Bwana alinichagua mimi nimtumikie na niwe binti yake mpendwa.

Changamoto: Kama Yesu alivyomgundua mwanamke aliyekuwa katika mateso, uwe makini kwa wale wanaokuzunguka wanaojisikia hawana thamani. Washirikishe kwa namna binafsi kwamba Yesu alibadilisha hali yako kutoka kuwa aliyetengwa na ‘asiye msafi’ kuwa mtoto wa Mungu mwenye thamani.

Maombi: Bwana, tusaidie tuone watu waliotengwa walio karibu nasi na utupe ujasiri wa kuwafikia tuwashirikishe uzoefu wetu binafsi wa uhuru na uponyaji ulio ndani yako.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org