Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 3 YA 31

Isaya ni nabii wa Agano la Kale ambaye maneno yake yanamwonyesha Yesu. Miaka mamia mapema, Hana alisema, ‘...Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, na matendo hupimwa na yeye kwa mizani’ (1 Samweli 2:3). Miaka mamia baadaye, Mariamu alitoa unabii, ‘Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa hao wanaomcha’ (Luka 1:50).

Matamko ya Isaya, Hana na Mariamu ya haki ya Mungu yanatoka katika mila, wakati na hali tofauti kabisa. Lakini kila moja inaelekeza kwa Kristo anayekuja kuleta amani na mpangilio sahihi.

Kama mtu angevunja na kuingia nyumbani kwako, ungebadilisha ‘mambo yakae sawa mara tena’ ungetafuta haki na kisha ujenge upya. Ni kwa njia hiyo hiyo, Yesu alikuja kubadilisha dunia ‘ikae sawasawa tena’, akaleta haki na kutualika sisi tuijenge upya dunia pamoja.

Sauti yako ya unabii inaungana na ile yao, kama utauishi ukweli wa mabadiliko ambao Mungu amekuwekea mbele yako.

Changamoto: Ava DuVernay anasema, ‘Kuwa msanii, unalazimika kufikiria na kuumba na kujenga dunia. Kuwa mwanaharakati, unalazimika kufanya vivyo’. Ubunifu uliotumika unawezaje kukusaidia kushinda ukosefu wa haki?

Maombi Yesu, fanya kusudi la uumbaji wako liwe wazi kwa kuleta tumaini duniani. Nionyeshe wapi niungane nawe katika kujenga upya na kurejesha, ili tuwe ‘njia sahihi’ mara tena.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org