Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 11 YA 31

Kama msichana nikikua, nilikuwa nahudhuria mipango ya wanawake kanisani kwetu – Chama cha Wanawake – pamoja na mama yangu, aliyekuwa Katibu cha Chama cha Wanawake.

Familia yetu haikuwa tajiri, lakini nilitambua kwamba kila mara mama yangu alikuwa na moyo wa huruma na wa kuwajali wengine. Niliangalia akiwapa mara kwa mara chakula na maji wale wahitaji, kati ya vitu vingine, wakati bidhaa za serikali zilipopungua. Nilijenga haya maishani mwangu vile vile, nikifuata mfano wake. Najaribu kuwapa watu zawadi na vitu katika matendo ya wema, chakula cha moto, hata inapolazimu mimi nisile.

Mama yangu vile vile alikuwa na roho ya uombaji ambayo ilinivutia. Kwa hiyo nilifuatisha ufundi wa kuwaombea watu, vile vile kama mama yangu. Nilipotawazwa na kuagizwa kama afisa wa Jeshi la Wokovu, nikawa ‘Mwombezi Mwaminifu’! Nimeanzisha mtandao wa maombi kwa kutumia mtandao wa kijamii na baruapepe kuwashirikisha wengine kuwakilisha mahitaji yao mbele za Bwana.

Kama jinsi Waebrania 13:2 inavyotukumbusha sisi: ‘Msisahau kuwafadhili wageni, maana kwa ajili hii, wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.’

Changamoto: Hebu sisi sote tuwe na moyo wa kumjali kila mmoja kwa sababu hatujui jinsi tutakavyogusa maisha tunaposhirikiana nao. Mruhusu Mungu akutumie kama chombo chake katika eneo hili la huduma.

Maombi: Bwana, naomba mkono wako wa upendo, rehema, neema, amani na hekima viwe juu yetu tunapotafuta kuhusika kutetea haki ya jamii. Tusaidie tuwe tayari kuomba kwa, ajili ya wengine na kusimama katika nafasi kwa wale wanaohitaji msaada wetu. Katika jina la Yesu. Amina.

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org