Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 14 YA 31

Mathayo 25:40 inaangazia jambo muhimu: inajenga daraja kati ya matendo yetu kwa wengine na utumishi wetu kwa Mungu.

Katika kazi yangu ndani ya Jeshi la Wokovu, Kanisa la Kimataifa la Kikrito na la hisani, tunatetea na kujaribu kuwa waleta mabadiliko katika jamii zetu. Wakati mwingine tunalaumiwa kwa kutokuwa wainjilisti wa kutosheleza au wanaofanya kazi upande mmoja wa utume wa Jeshi la Wokovu peke yake duniani.

Kifungu hiki kinatoa changamoto kwa sauti hizi na kinaleta mtazamo juu ya matendo ya haki yetu ya jamii. Hapa, yamefumwa na kuonekana kama utumishi kwa Mungu, na sio tu matendo mema kwa watu wanaonufaika nayo. Mwito wako wa kuleta mabadiliko unachangia katika Ufalme wa Mungu. Naamini wakati matendo yetu yamefungwa katika maombi hutufanya sisi ‘kuwajibika’, na Ufalme wa Mungu na Neno lake linakuja kujulikana na kusambaa kwa wote kulisikia na kulipitia.

Changamoto: ‘Nimeokolewa Kutumika’ ni maneno yanayozoelewa katika utume wa Jeshi la Wokovu. Yanatupa changamoto namna gani ya kuchukua mwito kutoka katika kifungu hiki? Matendo na maneno yetu yanawezaje kuwa mbegu za mabadiliko pale tunapoishi?

Maombi: Bwana, chukua yote niyafanyayo na uyafanye yako.

Andiko

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org