Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 17 YA 31

Nafanya kazi huko Wageningen, jiji la uchangamfu la chuo kikuu huko Uholanzi pamoja na watu kutoka katika mila na desturi mbalimbali.

Hapa, nimetambua kwamba wakati wa kufanya kazi kama mwanzilishi katika kile kiitwacho ‘Kujieleza Upya’, (Fresh Expression) na tunaimba, tunacheza na kushirikishana hisia zetu za ndani, tunajenga mshikamano maalum mmoja na mwingine. Ni kama Kristo yupo hapo pamoja nasi, akijaza mioyo yetu joto na faraja.

Kuimba na kucheza ni mambo yenye nguvu sana kwa wamama vijana ambao mara nyingi hujisikia kutengwa. Shughuli hizi hujenga madaraja kwenye vikwazo vya lugha, zikiwaruhusu wanawake kuungana na kushirikishana furaha, hata kama hawazungumzi lugha moja. Kupitia kwenye nyakati hizi za furaha, wanaweza kusahau kuhusu upweke na kuwa katika nchi ngeni au mashaka yanayokuja na changamoto za mazingira ya nyumbani.

Kwangu, muunganiko huu unaonyesha uwepo wa Mungu katikati yetu, kuonyesha sisi ni familia moja chini ya malezi yake. Ni mwonekano mdogo wa Ufalme wa Mungu hapa duniani, mahali ambapo kila mmoja alipo, na upendo wake unaangaza kupitia kwa kila moja ya mwingiliano.

Changamoto: Angalia kila ambacho kinagusa moyo wako na karama gani aliyokupa Mungu. Hii itakuwezesha, kama Yesu alivyofanya, kushirikishana upendo wa Mungu na wengine, hata kama lugha zetu au utamaduni vinatofautiana. Mara nyingi, sio maneno bali tabia ya wazi, kama aliyokuwa nayo Yesu.

Maombi: Mungu, twaomba utulete pamoja katika umoja. Hebu tupate kwako nguvu za kufanya mema tunapofanya kazi katika maeneo yetu duniani. Tusaidie kufuata mfano wa Yesu, wakati wote tuwe tayari kuwasaidia wale ambao unawaleta kwetu.

Andiko

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org