Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 21 YA 31

Katika maisha, tunakua tukisikia kuhusu sheria kuu ‘Na kama mnavyotaka watu wawatendeeni ninyi, watendeeni vivyo hivyo.’ (Luka 6:31). Kila mara nilifikiri ni maneno watu walikuwa wanasema ili watoke katika kutendewa bila haki. Sikufahamu kwamba ilikuwa ni amri ya kutoka katika Biblia.

Kama mchungaji mseja wa kike, nimekutana na haja ya kutumia kifungu hiki kwa manufaa yangu mwenyewe, nikikirudia kwa wale wanaonizunguka walionitendea kinyume na haki kwa sababu ya hali na jinsia yangu. Lakini sikufikiria Luka alikuwa anasema nini kwa kweli: ‘Wapende maadui zako, watendee mema wale wanaokuchukia.’ Mara nyingi tafakari yangu juu ya vifungu hivi ilikuwa katika hali ya uchoyo.

Kristo aliteseka kwa ukosefu wa haki mara nyingi, na bado aliwapenda wengine, aliwaponya na akawasamehe wale waliomtesa. Je, hatutakiwi kufanya vivyo?

Katika safari za hivi karibuni, nimejifunza kukumbatia utamaduni, lugha na nchi, nami nimependa kila dakika, lakini nimekutana na dhihaka, mizaha na uonevu. Hata hivyo, kwa kuzingatia huduma ambayo Mungu amenipa kwa kuniamini, nimejifunza kuomba, kupenda na kusamehe kama ninavyoshuhudia mabadiliko ambayo Mungu anayafanya katika maisha ya wale wanaonitesa mimi.

Changamoto: Kamata mtazamo kuhusu nini kinatendeka kwako, na ukumbatie ujumbe wa Luka 6:27-36, pamoja na Mika 6:8.

Maombi: Mpendwa Baba wa Mbinguni, tupe moyo wa kupenda na kuwa na wema kwa wale wasio wema kwetu. Tusaidie tukumbuke kila mara sheria kuu na tutende kwa haki, na tuwe na rehema, kama ulivyo wa rehema, bila kutarajia chochote kama malipo. Katika jina la Yesu. Amina.

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org

Mipango inayo husiana