Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 20 YA 31

Pamoja na matatizo yote yaliyopo kati ya Wayahudi na Wasamaria, Yesu alisema kwamba ni lazima yeye aende kupitia Samaria.

Kusudi lake la kweli lilikuwa kukutana na mwanamke mmoja maalum, anayekutana naye kisimani na akamwomba maji. Kama tukisoma Yohana 4:1-20, tunajifunza kwamba Yesu alikabiliana na mwanamke, akamfanya ajisikie wa muhimu, na akachukua muda kuzungumza naye kuhusu uzoefu wa maisha yake. Ni katika wakati huo mwanamke akatambua kwamba hashughuliki na mtu wa kawaida wa Kiyahudi – mtu huyu ni wa tofauti.

Yesu alipouliza kuhusu maisha ya nyuma ya mwanamke, anaonekana kuona aibu na anabadilisha mazungumzo yatoke kwenye hadithi binafsi na anazungumzia kuhusu sehemu za ibada. Bila kukwepa au kuona aibu, Yesu anamfanya mwanamke aone makosa yake. Anamwambia kwa uwazi kwamba sio kuhusu kuwa mahali sahihi, bali ni kuwa na moyo sahihi. Baadaye, anamdhihirishia kwamba yeye ni Masihi (Yohana 4:26).

Bila kujali tuna dhambi kiasi gani, au tunafikiri kwa chini kiasi gani sisi wenyewe, Mungu anatupenda naye anatuita tumwabudu katika njia sahihi. Hii ni picha nzuri ya jinsi gani kuwatendea wengine kwa haki, na kwa heshima inavyoonekana na kuwafahamisha wengine thamani yao wenyewe.

Changamoto: Hebu tumwabudu Mungu katika njia sahihi, tukiwa na upendo wa kujitoa kwa Mungu na kwa majirani zetu. Je, kuabudu kwako ni halisi na kwa uaminifu, bila ya kuwa na makusudi yaliyojificha au uchoyo?

Maombi: Bwana, nisaidie nikwabudu kwa uaminifu kamili, ili niwatendee wengine kwa heshima wanayostahili, hata wakati mawazo yao ni tofauti na yangu.

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org

Mipango inayo husiana