Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 19 YA 31

Ndani kabisa ya moyo wa kila mwanamke ipo hamu ya haki, katika dunia ambayo wema unadumu.

Huku, tukiona dunia ambayo imegubikwa na mgogoro, na vilio vya kutaka msaada mara nyingi vikipuuzwa. Vita vya Myanmar vimeloanisha udongo kwa damu ya wasio na hatia, na kutusukuma sisi kufikiria ‘Ni nani jirani yangu?’ (Luka 10:29). Jitihada hii ni zaidi ya vichwa vya juu vya habari, ni hadithi ya kuangamiza maisha yaliyovurugika na ndoto zilizoharibiwa.

Kama waamini, mioyo yetu inaumia kwa ajili ya majirani zetu huko Myanmar, wanaoteseka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya ukatili, vikiacha mamilioni wamehamishwa na maisha yameharibiwa. Jirani yetu ni mama huko Myanmar, anayemkumbatia mwanae wanapotorekea porini kwenye usalama. Ni baba, anayehuzunikia kupotea kwa mkewe, na watoto ambao kutokuwa na hatia kwao kumeibiwa na ukatili wa bila kukoma wa vita. Uchungu wao unatuita sisi, ukitutaka tubebe upendo wa Kristo na tutafute haki kwa ajili ya majirani zetu duniani.

Changamoto: Kumbatia mwito wa Luka 10:27; upendo unavuka mipaka. Chukua hatua sasa – omba, tetea wale wenye mahitaji. Acha tuungane kwa huruma, tutafute haki na amani kwa ajili ya majirani zetu duniani.

Maombi: Bwana, wavute katika rehema yako wale wanaoteseka. Wafariji wenye huzuni, watie nguvu waliojichokea, wahamasishe waoga. Wakinge wasio na hatia, watengeneze waliovunjika na waendeleza wote katikati ya vurugu.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org