Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 22 YA 31

Nilimpoteza baba yangu nilipokuwa na umri mdogo. Nilimtizama mama yangu mjane akilia kwa ukimya alipokuwa anazidiwa na mahitaji ya kuwalea watoto watatu wadogo peke yake.

Tulipokuwa tunapitia huzuni yetu, tulishughulikia maneno yasiyo ya wema yaliyoambatana na ubaguzi kutoka kwa wengine. Tulitendewa tofauti na zamani. Sauti zetu zilipuuzwa kwa sababu tu hatukuwa na baba na mume. Watu walituonea nasi tuliumizwa sana na matendo ya wale waliotuzunguka.

Tulishikilia ahadi ya Mungu ipatikanayo katika Zaburi 68:5. Mungu alitupa nguvu na akatuvusha alipoponya taratibu majeraha ya ndani ya mioyo na akili zetu kutokana na kumbukumbu za maumivu ya jinsi tulivyotendewa. Ingawa tulijisikia tu wapweke, siku zote Mungu alikuwepo pamoja nasi.

Yeye ni baba mwenye huruma anayewapenda na kuwajali watoto wake wapweke. Yeye ni mlinzi imara anayewalinda na kutenda kwa niaba ya wajane wasio na uwezo. Wakati wote yupo hapo.

Changamoto: Tunawezaje kuonyesha kupitia kwa maneno na matendo kwamba Mungu ni baba wa wasio na baba na mtetezi wa wajane. Tunaweza kujibu namna

gani tunapoona yatima na wajane wenye maumivu, huzuni, upweke na wanao kandamizwa?

Maombi: Baba wa Mbinguni, tunashukuru kwa sababu ya upendo wako usio na masharti na huruma zako kwetu. Tusaidie Bwana, tuwashirikishe upendo na huruma hii kwa maneno na matendo na wale wenye mahitaji. Amina.

Andiko

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org