Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 26 YA 31

Zaburi 33 inasherehekea baadhi ya sifa za tabia ya Mungu – haki, na wema. Ni mwito wa kuabudu kwa yeyote atakaye mheshimu Mungu. Kifungu cha 4 na 5 vinaleta ukweli nyumbani kwamba Mungu anaweza kuaminika, kwani neno lake ni sahihi. Hakuna kosa au utovu wa haki ndani yake.

Israeli ilikuwa imepata ushindi dhidi ya adui. Mwandishi wa Zaburi anakiri kwamba ushindi huu usingepatikana bila ya Mungu kuonyesha yeye ni wa haki, ufalme wake unajengwa juu ya kanuni hizi (Zaburi 89:14). Katika kunyanyasika kwa Israeli, Mungu alijitokeza kuwakomboa watu wake kutoka kwenye kibano cha adui kwasababu ‘Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki na hukumu kwa wote wanaoonewa.(Zaburi 103:6).

Mara nyingi tunakabiliwa na ukandamizaji wa aina mbalimbali. Wakati mwingine sisi ni waathirika wa ukosefu wa haki, na wakati mwingine tunamjua mtu ambaye anatendewa bila haki. Mungu anayafahamu. Kama tukijinyenyekeza kwake, ataongoza njia zetu kwa namna ambayo italeta uhuru kwa wanaokandamizwa. Mwache Bwana, yeye huwaweke huru waliofungwa na huwafunga waliovunjika mioyo. Mwamini yeye naye ataleta haki – inaweza kukawia, lakini hakika itakuja.

Changamoto: Je, unakabiliwa na ukosefu wowote wa haki au unamjua yeyote ambaye yupo katika hali hiyo? Mika 6:8 inasema: ‘Ee mwanadamu yeye amekuonyesha yaliyo mema, na Bwana anataka nini kwako ila kutenda haki, na rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako’. Juma hili, omba kwa ajili ya ujasiri mtakatifu uweze kusimama kwa ajili ya lile lililo la haki na mara nyingi uwasaidie wanaokandamizwa.

Maombi: Bwana, kama ulivyo, ndivyo nilivyo katika dunia hii. Nisaidie nilete nuru na tumaini kwa wale wanaonizunguka mimi wanaoihitaji zaidi.

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org