Tafakari Kuhusu HakiMfano
Kwa kuwa alikuwa na waamini ndani ya kanisa Filipi, Paulo alifahamu vema maisha yao. Vile vile alipokea ripoti ya jinsi wanavyoishi. Akiwa na huo uelewa aliwaandikia, wasiangalie tu matakwa yao wenyewe, bali wawafikirie wengine.
Kwa maneno mengine, aliwaonya wasiwe wachoyo. Wasiache malezi na umakini wao utekwe jumla kwa kujiangalia wenyewe au kuziangalia familia zao wenyewe. Waanzishe hamu laini ya furaha ya wote na kuacha ustawi wa wengine uwe karibu sana na moyo wako. Hii, bila shaka, siyo kwamba pawepo na kuingilia kiholela shughuli za wengine, au kwamba tuwe na mwenendo wa kuwa na shughuli nyingi katika maswala ya wengine, bali kwamba tuchukulie kwa makini ustawi wa wengine, na tujitahidi kuwatendea mema.
Wajibu wetu, kwa pamoja. Hakuna aliye huru kuishi kwa ajili yake mwenyewe, kupuuza mahitaji ya wengine. Tumeitwa kuvunja roho nyembamba ya uchoyo, na badala yake tuweke upendo na fadhili tukithamini furaha ya wengine.
Changamoto: Mara ngapi umehusika mwenyewe na matakwa ya wengine? Unajali? Unasaidia? Anza na maombi.
Maombi: Bwana, asante kutuumba tuwe sehemu ya familia na jamii. Tusaidie tusitizame tu matakwa yetu wenyewe, bali tuangalie vile vile matakwa ya wengine. Hatuwezi kufanya bila ya msaada wako, kwa hiyo tafadhali uwe pamoja nasi. Katika jina la Yesu. Amina.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org