Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 29 YA 31

Tunatakiwa kutambua kwamba kujitoa kwa Wakristo wa mwanzoni hakukusababishwa na ubinadamu. Mwito na huruma yetu kuhudumu na kuwajali wale wahitaji ni kusudi lililo ndani ya kiini katika mafundisho ya Biblia.

Waisraeli walichagua kuwatunza maskini kati yao kwa sababu walitambua Mungu anawajali maskini. ‘Kama akiwepo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmoja wapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini, lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiyo.’ (Kumbukumbu ya Torati 15:7-8). Tunapokea amri ya Mungu kwa watu wake na kufanya uchaguzi wa kutii.

Mungu ana moyo kwa maskini naye anataka sisi tuwe na moyo huo huo. Watu wengi pamoja na Wakristo, huwadharau wale wenye mahitaji, hawaamini kwamba wana kitu cha kuchangia katika jamii. Tunatakiwa kutambua kwamba akili hii ni dhambi. Mungu anasema tunatakiwa kuwa wema kwa wahitaji na kuwatendea maskini kama kaka na dada zetu katika Kristo.

Dhana ya haki ya kibiblia inafunika zaidi ya adhabu kwa kufanya mabaya. Inajumuisha kuchukua msimamo wa kuwatendea watu wote kwa usawa, kuwalinda na kuwajali. Mungu anawaita watu wote kutafuta haki kwa wale walio katika mazingira hatarishi ya mateso na ya ukosefu wa haki. Biblia inaweka pamoja haki na kutenda kwa usawa na kuwa na mwenendo ambao ni wa rehema, kuwa mtu ambaye anatoa upendo, wema na huruma.

Changamoto:‘Tunapokuwa na nafasi ya kumsaidia mtu mhitaji, tuna nafasi ya kumtumikia Yesu.’ Hii inabadilisha namna gani jinsi utakavyoweka katika matendo kuishi kwa haki?

Maombi: Mpendwa Bwana, tunaomba umwage neema yako nyingi na rehema juu ya wote wenye mahitaji. Tunaomba uwape nguvu na ujasiri wa kuvumilia, na uwaletee amani ipitayo fahamu zote.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org