Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Somo la leo labeba "Ole" tatu kati ya saba zilizotamkwa dhidi ya Mafarisayo na waandishi. Yesu anabainisha wazi kabisa unafiki uliokithiri katika matendo na mienendo yao. Ni onyo juu ya hatari ya kupatwa na hukumu ile inayowakabili wote wanawapotosha watu kwa mienendo yao wasiingie katika Ufalme wa Mbinguni. Je, maneno haya yanatufundisha nini mimi na wewe? Ni muhimu sana kwetu sote kutumia dhamana ya kufundisha watu njia ya Mungu, tukitenda kwa uaminifu na kuwa mfano wa kuigwa. Ndivyo Paulo alivyoishi, maana katika Flp 3:17 anasema,Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz