Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Matendo mema na usafi wa nje ni sawa, lakini haya hayawezi kutupatia kibali mbele za Mungu. Kile kiujazacho moyo ndicho kinachoelekeza hatima ya mtu. Ndani ya moyo ndipo penye mipango yote ya maisha ya mtu. Dhambi hubuniwa ndani ya moyo. Hiyo humtia mtu unajisi. Usafi wa kiroho pia huanzia moyoni. Hilo humpatia mtu haki. Hivyo changamoto ya kila Mkristo ndiyo hii: Namna gani ya kuulinda moyo wake ili asifanane na wale Mafarisayo na waandishi waliojali mambo yanayoonekana, wakaacha yale ya imani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz