Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 13 YA 31

Hekalu lilikuwa fahari ya Wayahudi. Kwa mfano katika Lk 21:5 tunasoma kuhusuwatu kadha wa kadha walikuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu.Na waumini wa Agano la Kale waliweza kuimba juu ya uzuri wake namna hii:Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu(Zab 84:10). Hekalu liliashiria uhusiano wao na Mungu, na ndani yake walionana na Mungu. Wanafunzi walilionea shauku. Lakini Yesu alitabiri kuwa siku moja litabomolewa; nalo lilibomoka mwaka 70 BK. Bwana anaeleza pia dalili za nyakati za mwisho. Je, umegundua dalili kuu na ndogo za kurudi kwa Yesu mara ya pili katika somo la leo? Tunaposoma na kuona dhahiri dalili hizi zikitimia, hatuna budi kujiandaa kwa kuja kwa Kristo Yesu kwa kudumu ndani ya imani katika Yeye.

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz
 

Mipango inayo husiana