Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 7 YA 31

Jana tuliona makundi mawili wakimjaribu Yesu kwa nyakati tofauti. Leo wanaungana kupata nguvu zaidi. Lakini Yesu anatumia hali hiyo tena kuwafundisha kuwa imewapasa kumpenda Mungu na wanadamu. Namna gani tunaweza kumpenda Mungu na jirani zetu? Tafakari Yesu anavyosema katika m.37-40:Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii. Kisha Yesu anawaonyesha kuwa yeye ni Mwana wa Mungu; ndiye aliyetabiriwa katika unabii. Kwa hiyo walipaswa wamwamini badala ya kumchukia. Yesu Kristo ni mmoja na Baba, yaani Mungu. Kumpinga na kumchukia Yesu ni kumkataa Mungu.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz
 

Mipango inayo husiana