Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Sadaka ya dhambi ililetwa kwa makosa yaliyotendwa pasipo kukusudia, lakini baadaye yalijulikana. Sadaka hii ilifanya utakaso wa dhambi kwa mtu binafsi, kundi la waumini, au kiongozi. Hakuna mtu aliye kamili, sisi sote ni wakosaji. Hata hivyo tunaweza kumtumikia Mungu mtakatifu. Ebr 9:11-14 inaeleza hiyo inawezekana kwa namna gani:Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?- Ng’ombe mzima wa sadaka alichukuliwa nje ya kambi na kuchomwa moto hapo. Hulingana na Yesu alivyouawa nje ya lango la mji wa Yerusalemu. Ni ishara ya kuondolewa dhambi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz