Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

SIKU 5 YA 30

Somo linaeleza utaratibu wa sadaka ya dhambi kwa “mtu awaye yote” asiye kuhani wala kiongozi wa serikali. Njia ya kutakaswa ilikuwa wazi kwa wote, haijalishi kama hali zao zilikuwa duni kiuchumi. Hata waliruhusiwa kwenda na nafaka badala ya kondoo au mbuzi. Lakini damu ilihitajika kwa sadaka ya dhambi. Kwa hiyo unga uliteketezwa kwa kuchanganywa na sadaka nyingine ya nyama, kama ilivyoelezwa katika 5:12:Kuhani atatwaa konzi yake ya huo unga kuwa ukumbusho wake, na kuuteketeza juu ya madhabahu, juu ya sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto; ni sadaka ya dhambi. Katika Ebr 9:22 imeelezwa jinsi damu ya Kristo ilivyo sadaka pekee ya kuondoa kabisa dhambi hata leo: Katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.Tafakari pia ilivyoandikwa katika Ebr 10:1-10:Torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao. Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz