Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Taifa linawategemea sana viongozi ambao hapa wanawakilishwa na wakili Shebna. Lakini mtumishi huyu hakuwa tofauti na watu wengine wa Yerusalemu. Badala ya kuwashauri na kuwaongoza wenzake wamtumaini Mungu, akaungana nao katika kutegemea msaada kutoka mataifa mengine yasiyomcha Mungu. Shebna aliongoza watu kupuuza ujumbe wa nabii Isaya. Wote wasiomtii Mungu hawadumu. Wanaachwa wasimtumikie; badala yake Mungu anawainua wengine mahali pao. Wewe usikengeuke wala usishiriki kuwapotosha watu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz