Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Nyenyekeeni chini yamkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenuzote, kwa maanayeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu(m.6-7). Neno hili niagizokwako unayetaka kujitafutia mwenyewe utatuzi wa mambo yako. Tena nifarajakwako uliyekwama katika hali ngumu ya maisha yako. Mungu ni BABA yako! Yeye ni mwepesi sana kutoa kuliko wewe kuomba! Tena hashindwi uwezo wa kukusaidia! (Maelezo:Silvano= karani wa Petro.Babeli= mji wa Rumi).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz