Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 28 YA 31

Kwa kifo cha Yesu tumekwisha okolewa na dhambi, kwa hiyo tufuate mapenzi ya Mungu:Msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani(m.2). Leo tunafafanuliwa zaidi maana ya kuishi katika mapenzi ya Mungu.Mkeshe katika sala, Petro anaandika katika m.7.Tupendanekwa juhudi nyingi! Tukifanya hivyo hatuwezi kusengenyana bali tutasameheana.Iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi(m.8). Petro anaendelea kuandika:Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika,bali kwa furaha; yaani tuwe na ukarimu (m.9). Kila Mkristo ameipokeakaramayake. Isimfanye ajivune, bali kama Petro anavyoandika:Itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu, nakwa kadiri alivyoipokea karamakila mmoja(m.10). Na shabaha kuu ni kwambaMungu atukuzwekatika yote (m.11)!

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz