Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Petro huwatia moyo Wakristo wenye taabu. Kwanza anarudia kusema kwambamsione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho, maana Kristo naye aliteswa (m.12). Pili anawaambia jambo la ajabu kwambawafurahi:Kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini(m.13a). Maanamkilaumiwa kwa ajili ya jina la Yesuni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia(m.14). Zingatia maneno ya Yesu:Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo(Lk 6:22-23). Kwa hiyo tunasoma hivi kuhusu Mitume: Kutokana na ushauri wa Farisayo Gamalieli, baraza la Kiyahudiwakakubali maneno yake; nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao. Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo. Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo(Mdo 5:40-42). Wakristo wako heri kwa sababu tatu:1.Ni dalili kuwa Yesu kweli yuko ndani yao.2.Roho wa Mungu huwatia nguvu na ujasiri (m.14:Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.Ukipenda, linganisha na Mt 10:17-22).3.Wana thawabu kubwa Mbinguni!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz