Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Mtume Petro anawaagiza tena Wakristo wawe na mwenendo mwema! Makusudi ya kuwa na mwenendo mwema ni yafuatayo:1.Kupata maisha mema (m.10:Atakaye kupenda maisha, na kuona siku njema, auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila).2. Kuwa karibu na Mungu (m.12:Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao).3.Kumshuhudia Yesu Kristo mbele ya wasioamini (m.15-16:Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo). Nguvu ya kuishi maisha haya tutapataje?Mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu(m.14). Yaani, tuendelee kumkabidhi Yesu maisha yetu, maana tuko ndani yake (m.16: Tunamwenendo wenu mwema katika Kristo). Tuendelee kukiri makosa yetu na kusafishwa katika damu yake. Tumwogope yeye kuliko binadamu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz