Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 27 YA 31

Hapa kuna mafundisho mawili:1.Kristo alipata mateso, kwa hiyo sisi wafuasi wake tusishangae nasi tukipata mateso.Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile(m.1a). K.m. tutakuta matukano kwa sababu yakutokwenda mbio pamoja[na wasioamini]katika ufisadi.Wakiwatukana”, Petro anaongeza katika m.4. Maana wale tulioshiriki nao katika maisha ya dhambi hutaka turudi kwao na kuwa kama wao tena. Tabia mpya tumeiona na kujifunza kwa Yesu.Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake(2:21). Yesu anatutia moyo namna hii:Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka(Yn 15:18-21).2.Tumeshaachana na dhambi, maana Kristo aliteswa badala yetu kwa ajili ya dhambi zetu. Matokeo yake Petro anayafafanua hivi:Aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi(m.1b).Yesumwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa(2:24). Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa(3:18). Katika Rum 6:5-11 jambo hilohilo linafafanuliwa zaidi: Kama mlivyounganika naye[Yesu]katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Dhambi zetu zilichukuliwa na Yesu msalabani, kwa hiyo hazina haki wala nguvu ya kututawala tena!

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz