Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Kuanzia mlango huu wa kitabu cha nabii Isaya, Mungu anatangaza hukumu kwa mataifa yote yasiyomjua yeye. Ujumbe wa fungu hili unahusu taifa lote la Babeli. Kuanguka kwa wapinzani wa Mungu ni kuleta amani na uhuru kwa watu wa Mungu. Nguvu za Babeli ni za kitambo tu. Taifa hili lilimkataa Mungu. Wasiomjua Mungu ni maadui. Ndio hawa ambao huwatesa wakristo. Katikati ya kukata tamaa kuna matumaini. Wanaomtegemea Mungu wanawavuta wengine wamjie Yeye. Usitegemee watu, hawana nguvu. Umtegemee Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz