Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Uovu unaondoa heshima na utukufu wa watu. Vikwazo vinavyowazuia watu vina mwisho wake. Kuondolewa kwa mateso kunafungua mlango wa kuishuhudia kazi ya Mungu. Watu na mataifa yanayojitwalia heshima kwa manufaa yao wenyewe hawadumu milele. Mungu ameamua kuiondoa kabisa hali hiyo. Ana lengo la kuwakomboa watu wake kutoka hali ya kukandamizwa, kupuuzwa na kudharauliwa. Mungu anataka kila mtu amrudie Yeye, na aishi kwa kuzingatia nia ile iliyokusudiwa na Mungu tangu uumbaji:Siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli. Wala hataziangalia madhabahu, kazi ya mikono yake; wala hatavitazama vilivyofanyika kwa vidole vyake, maashera na sanamu za jua(m.7-8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz