Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Mungu anatumia njia nyingi katika kufikisha ujumbe. Isaya anapewa agizo na Mungu na analitii. Agizo hili ni kuwahubiria mataifa kwa kutembea uchi. Maisha yake yawe kielelezo au picha halisi ya hali itakayotokea kwa taifa lolote lisilomcha Mungu. Nabii anabeba tabia na uovu wa jamii. Watu wasiomwamini Mungu, wale wanaotumainia enzi na mamlaka zao, tena kujikweza na mafanikio yao badala ya Mungu, mwisho wake watadhalilishwa na Mungu mwenyewe. Mungu anapenda mtumishi ashiriki maumivu ya jamii. Kumbuka Yohana Mbatizaji asemavyo kuhusu Yesu kwamba ndiyeMwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu(Yn 1:29).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz