Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 10 YA 31

Mbele ya Mungu hata wanaojigamba kuwa ni mashujaa na mashuhuri hugwaya na kutetemeka, kwa kuwa Mungu ndiye sababu ya kuwepo kwa watu. Mafanikio ya maisha huanzisha uwezekano wa kuabudu miungu. Mungu ameamua kuondoa majigambo. Atayaondoa haya kwa njia ya kumleta Mwokozi. Kusudi kuu la Mungu si kuangamiza bali ni kuokoa. Kuokoa kunaambatana na kuponya. Taifa linapookolewa linakuwa kiini cha majirani zake kumtambua Mungu na kisha kumfuata. Mungu ameleta uumbaji mpya. Mataifa yote yamwelekee yeye.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz