Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 9 YA 31

Kila taifa linapewa ujumbe maalumu kutoka kwa Mungu. Ujumbe unatolewa kufuata tabia, historia na mazingira ya eneo linalohusika. Uovu unaotendwa unategemea mambo hayo. Taifa la Misri lilijivunia na kutegemea mto Nile. Nguvu ya kiuchumi inategemea mazao ya mto huu. Nguvu hii ya kiuchumi ilizaa kiburi. Lakini kuimarika huku kutatoweka. Mungu anataka kuonesha nguvu zake kwa kuidhoofisha Misri. Mungu anashusha kiburi na majivuno. Njia ya kujiepusha na kushushwa ni kumrudia Mungu na kumtegemea yeye.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz