Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 4 YA 31

Jambo linaloonekana wazi katika somo la leo ni ahadi itokayo katika kinywa cha Mungu. Ahadi hii ni kwamba Mungu anainuka ili akupiganie. Amesimama mahali pako. Hakuna Mungu wa aina hii nje ya Ukristo. Imani ya Kikristo ndiyo pekee hapa duniani inayokiri juu ya kuwepo kwa Mungu anayesimama kumtetea mtu na kumkomboa. Kwa nini Mungu analeta ahadi hii ya furaha na amani kwako wewe, tena wakati huu katika maisha yako? Ni kwa sababu ameyaona maisha, mateso, mahitaji na maisha yako. Kristo Yesu anakuita:Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi (Mt 11:28-30).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz