Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Utukufu na umaarufu wa watu unapungua na kufutika kabisa. Wenye nguvu huja na kwenda. Mambo ya watu hupita yote, bali mambo ya Mungu yasimama. Neno la Yesu ndilo hukaa milele. Kiburi na majivuno huzuia baraka za Mungu na kuleta maangamizi.Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa (Mt 23:12). Kuna mbinu gani za kuzuia majivuno uliyo nayo? Mbinu sahihi ya kuyaondoa haya na kuyashinda ni kuwa mnyenyekevu. Unyenyekevu wa kweli unajaa pendo linalotoka kwa Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz