Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Hili ni neno hasa kwako uliye mchungaji, mwinjilisti au kiongozi wa aina nyingine katika kanisa. Ni ujumbemuhimu sanakwako kutoka kwa Bwana, maana Petro hutumia neno hili “nawasihi”. Tena anawakumbusha kuwa yeye ni nani:Mzeekatika kanisa,shahidi wa mateso ya Kristo,namshirika wa utukufuwa Mbinguni (m.1). Ujumbe wake ni kwambajambo kuukwa kiongozi liwe kuwaokoa watu wafike Mbinguni! Wala jambo kuu lisiwe kujinufaisha mwenyewe na kutaka cheo! Pima utumishi wako ukisoma anavyosema Yesu:Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake(Mt 16:24-27).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz