Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 26 YA 31

Mtume Petro hachoki kusema juu ya wokovu ulio katika Yesu Kristo. Sisi wahubiri wa Injili tufuate mfano wake katika huduma yetu ili watuwamwoneYesu na kumwabudu na kumpenda! Ubatizo unatuokoa, kwa sababu unatuingiza katika safina ambayo ni Yesu (m.21:Mfano wa mambo hayo[kuhusu safina na Mungu alivyookoa siku za Nuhu]ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi). Ukiwa ndani ya Yesuyote yaliyotendeka kwake ni yako!Yaani kuteswa kwake na kufa kwakemara moja kwa ajili ya dhambi(m.18),kufufuka kwake(m.21) na kumiliki kwake akiwayupo mkono wa kuume wa Mungu, ... malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiiishwa chini yake(m.22). Maana alifanya yotekwa ajili yao wasio haki,ili atulete kwa Mungu(m.18)! Zingatia kwambaaaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa(Mk 16:16).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz