Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 24 YA 31

Wanawake na wanaume niwarithi pamoja wa neema ya uzima(m.7). Yaani kwa upande wa wokovu wako sawa kabisa. Lakini kwa upande wa wajibu na nafasi katika nyumba, wako tofauti. Mume hawezi kuwa na nguvu na kujisikia mwanamume kweli, kama mke wake asipomheshimu na kuwa na utii. Vilevile mke hawezi kuwa na nguvu na kujisikia mwanamke kweli, kama mume wake asipomheshimu na kumpenda. Wasipotimiza wajibu wao, maisha ya kiroho yanapata shidambele za Mungu.Kwa hiyokujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje ... bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo na thamani kuu mbele za Mungu(m.3-4). Vilevile kuomba kwao huweza kuzuiliwa. Kwa hiyo imeandikwa katika m.7:Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu ... kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe(m.7).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz