Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Huenda unapambana na dhambi maishani mwako. Huenda umeshindwa kuwa na tabia nzuri mbele ya mwajiri wako kama tulivyoona jana. Basi, sikiliza kwa makini habari njema ya leo:Yeyealizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti(msalaba);ili, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki.Yaani kwa kifo cha Yesu umekombolewa na nguvu za dhambi na Shetani! Kila unapomshukuru Yesu kwa ushindi huu, ndipo uvunjapo nguvu za giza na kupata nguvu ya Roho. Paulo anatuomba tukumbukeneno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena(Rum 6:6).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz