Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Wakati ni jambo muhimu sana katika hatua zote za maisha ya binadamu. Rais wa kwanza wa nchi ya Tanzania, hayati Mwalimu J. K. Nyerere, alipowahamasisha watu kujiunga na madarasa ya kisomo ya watu wazima alikaza: "Wakati ni huu". Maana wakati haupo tu, bali una mwisho. Kumbuka "wakati ukuta". Hatari inayotukabili ni kuutumia wakati vibaya kwa mambo yasiyofaa, na yasiyotupatia faida. Zingatia wito katika m.1-3.Siku ya wokovu ndiyo sasa.Leo ni wakati wa kumpokea, kumwamini na kumfuata Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
