Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Utoaji hulingana na kupanda mbegu shambani. Kile unachotoa na mavuno yake, vyote ni zawadi ya Mungu aliye mwenye ukarimu wote. Kwa hiyo tunasoma ahadi hii katika m.10:Yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu. Tukizingatia ahadi hii ya Mungu tunaelewa sababu ya Paulo katika m.15:Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo. Na Mungu anapotutajirisha hivyo kwa kila namna kusudi lake ni kwamba tufanane naye, yaani,mpate kuwa na ukarimu wote(m.11). Utoaji una matunda yake mema: Kwanza unakidhi mahitaji ya wapokeaji, kisha unampatia Mungu shukrani. Hata mtoaji ataombewa. Katika m.13 Paulo anawaambia Wakristo wa Korintho kwamba watuwanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote. Tafakari jinsi Paulo anavyofafanua utoaji kamautii … katika kuikiri Injili ya Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz