Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

SIKU 25 YA 30

Mlihuzunizhwa, hata mkatubu”, maana yake ni nini?Roho Mtakatifu hufanya kazi ya kuliwezesha Neno la Kristo kuichambua na kuipa changamoto mioyo yetu kwa kuikosoa. Itikio la kweli moyo uliokosolewa au kuonywa na Neno la Mungu ni toba:Huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti(m.10). ”Toba” ni kuhuzunishwa kwa sababu dhambi uliyotenda, kuiungama mbele ya Yesu na kupokea msamaha wake kwa imani. Halileti majuto, bali furaha ya wokovu, ujasiri wa imani, na bidii ya kumfuata Yesu ukiishi maisha ya kumcha na kumpenda Mungu.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana