Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Kunakipawa au karama ya utoaji. Paulo anatukumbusha kuwa hiyo inaendana na kutoa kwa hiari na moyo mkunjufu. Hawalazimishi Wakorintho kutoa, maana utoaji wa kikristo unasukumwa na upendo. Kwa Paulo ahadi si deni, bali ni wajibu mbele ya Mungu tuliopewa kutokana na wingi wa neema ya Mungu katika maisha yetu.Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema(m.8). Tena ni baraka kwa wale watakaonufaika na matoleo yetu. Je, wewe ni mtu anayekusanya au kutawanya kwa ukarimu? Rudia m.6 ukitafakari matokeo ya jibu lako kwa swali hilo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
