1
2 Wafalme 4:2
Neno: Bibilia Takatifu
Elisha akamjibu, “Nitawezaje kukusaidia? Niambie, una nini ndani ya nyumba yako?” Akasema, “Mtumishi wako hana kitu chochote kabisa, isipokuwa mafuta kidogo.”
Linganisha
Chunguza 2 Wafalme 4:2
2
2 Wafalme 4:1
Mke wa mmoja wa wana wa manabii akamlilia Elisha, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu, amekufa, nawe unajua alikuwa anamcha BWANA. Lakini sasa yule anayemdai anakuja kuchukua wanangu wawili kama watumwa wake.”
Chunguza 2 Wafalme 4:1
3
2 Wafalme 4:3
Elisha akasema, “Zunguka kwa majirani zako wote ukaombe vyombo vitupu. Usiombe vichache.
Chunguza 2 Wafalme 4:3
4
2 Wafalme 4:4
Kisha ingia ndani na ujifungie mlango, wewe na wanao. Mimina mafuta kwenye vyombo vyote, na kila kimoja kinapojaa, kiweke kando.”
Chunguza 2 Wafalme 4:4
5
2 Wafalme 4:6
Vyombo vyote vilipojaa, akamwambia mwanawe, “Niletee chombo kingine.” Lakini mwanawe akajibu, “Hakuna chombo kingine kilichobaki.” Basi mafuta yakakoma kutiririka.
Chunguza 2 Wafalme 4:6
6
2 Wafalme 4:7
Yule mwanamke akaenda akamwambia yule mtu wa Mungu, naye mtu wa Mungu akasema, “Nenda ukayauze hayo mafuta ulipe madeni yako. Wewe na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachosalia.”
Chunguza 2 Wafalme 4:7
7
2 Wafalme 4:5
Yule mjane akaondoka na kujifungia ndani, yeye na wanawe. Wao wakamletea vyombo, naye akaendelea kumimina mafuta.
Chunguza 2 Wafalme 4:5
8
2 Wafalme 4:34
Kisha akapanda kitandani, akalala juu ya yule mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, macho yake juu ya macho ya mtoto, mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Naye alipojinyoosha juu yake, mwili wa mtoto ukapata joto.
Chunguza 2 Wafalme 4:34
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video