1
Mithali 3:5-6
Neno: Bibilia Takatifu
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.
Linganisha
Chunguza Mithali 3:5-6
2
Mithali 3:7
Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche BWANA ukajiepushe na uovu.
Chunguza Mithali 3:7
3
Mithali 3:9-10
Mheshimu BWANA kwa mali zako na kwa malimbuko ya mazao yako yote; ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.
Chunguza Mithali 3:9-10
4
Mithali 3:3
Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako.
Chunguza Mithali 3:3
5
Mithali 3:11-12
Mwanangu, usiidharau adhabu ya BWANA na usichukie kukaripiwa naye, kwa sababu BWANA huwaadibisha wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye.
Chunguza Mithali 3:11-12
6
Mithali 3:1-2
Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako, kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio.
Chunguza Mithali 3:1-2
7
Mithali 3:13-15
Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu, kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye.
Chunguza Mithali 3:13-15
8
Mithali 3:27
Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda.
Chunguza Mithali 3:27
9
Mithali 3:19
Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya dunia, kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake
Chunguza Mithali 3:19
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video