1
Kutoka 23:25-26
Swahili Revised Union Version
Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.
Linganisha
Chunguza Kutoka 23:25-26
2
Kutoka 23:20
Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokuandalia.
Chunguza Kutoka 23:20
3
Kutoka 23:22
Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.
Chunguza Kutoka 23:22
4
Kutoka 23:2-3
Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu; wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake.
Chunguza Kutoka 23:2-3
5
Kutoka 23:1
Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo.
Chunguza Kutoka 23:1
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video