1
Mwanzo 25:23
BIBLIA KISWAHILI
BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na makabila mawili ya watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.
Linganisha
Chunguza Mwanzo 25:23
2
Mwanzo 25:30
Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.
Chunguza Mwanzo 25:30
3
Mwanzo 25:21
Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.
Chunguza Mwanzo 25:21
4
Mwanzo 25:32-33
Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? Yakobo akamwambia, Niapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
Chunguza Mwanzo 25:32-33
5
Mwanzo 25:26
Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.
Chunguza Mwanzo 25:26
6
Mwanzo 25:28
Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo.
Chunguza Mwanzo 25:28
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video