1
1 Wakorintho 13:4-5
Biblia Habari Njema
Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya
Linganisha
Chunguza 1 Wakorintho 13:4-5
2
1 Wakorintho 13:7
Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.
Chunguza 1 Wakorintho 13:7
3
1 Wakorintho 13:6
hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.
Chunguza 1 Wakorintho 13:6
4
1 Wakorintho 13:13
Sasa yanadumu haya matatu: Imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.
Chunguza 1 Wakorintho 13:13
5
1 Wakorintho 13:8
Upendo hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita.
Chunguza 1 Wakorintho 13:8
6
1 Wakorintho 13:1
Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
Chunguza 1 Wakorintho 13:1
7
1 Wakorintho 13:2
Tena, naweza kuwa na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, nikafahamu siri zote na kujua kila kitu; naweza kuwa na imani yote hata nikaweza kuihamisha milima, lakini kama sina upendo mimi si kitu.
Chunguza 1 Wakorintho 13:2
8
1 Wakorintho 13:3
Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili wangu uchomwe, kama sina upendo hiyo hainifai chochote.
Chunguza 1 Wakorintho 13:3
9
1 Wakorintho 13:11
Nilipokuwa mtoto mchanga nilisema kitoto, nilifahamu kitoto, nilifikiri kitoto. Lakini sasa, maadamu mimi ni mtu mzima, mambo ya kitoto nimeyaacha.
Chunguza 1 Wakorintho 13:11
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video