1
2 Wafalme 4:2
Biblia Habari Njema
Elisha akamwuliza, “Sasa nikusaidieje? Niambie kile ulicho nacho nyumbani.” Mama huyo mjane akamjibu, “Mimi mtumishi wako sina kitu chochote ila chupa ndogo ya mafuta.”
Linganisha
Chunguza 2 Wafalme 4:2
2
2 Wafalme 4:1
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu amefariki, na kama ujuavyo, alikuwa mcha Mungu, lakini aliyemwia fedha amekuja kuwatwaa wanangu wawili wawe watumwa wake.”
Chunguza 2 Wafalme 4:1
3
2 Wafalme 4:3
Elisha akamwambia, “Nenda kwa jirani zako uazime vyombo vitupu vingi kadiri utakavyopata.
Chunguza 2 Wafalme 4:3
4
2 Wafalme 4:4
Kisha uende, wewe pamoja na wanao, mjifungie ndani ya nyumba, na muanze kujaza mafuta. Kila chombo mnachojaza, kiwekeni kando.”
Chunguza 2 Wafalme 4:4
5
2 Wafalme 4:6
Vilipojaa vyote, akamwambia mwanawe mmojawapo, “Niletee chombo kingine.” Mwanae akamjibu, “Vyote vimejaa!” Hapo mafuta yakakoma kutiririka.
Chunguza 2 Wafalme 4:6
6
2 Wafalme 4:7
Akarudi kwa mtu wa Mungu na kumweleza habari hizo. Naye mtu wa Mungu akamwambia, “Nenda ukauze hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wanao mtaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki.”
Chunguza 2 Wafalme 4:7
7
2 Wafalme 4:5
Akaenda na kujifungia ndani ya nyumba na wanawe na kuanza kumimina mafuta ndani ya vyombo.
Chunguza 2 Wafalme 4:5
8
2 Wafalme 4:34
Ndipo akajilaza juu ya mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, na macho yake juu ya macho ya mtoto na mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Na alipokuwa amekaa hivyo, mwili wa mtoto ukaanza kupata joto.
Chunguza 2 Wafalme 4:34
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video