Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Somabiblia Kila Siku 3Mfano

Somabiblia Kila Siku 3

SIKU 21 YA 31

Bado kitambo kidogo” ni maneno yatumikayo mara saba katika somo hili. Yaweza kuwa na maana tano tofauti. Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni(m.16) inaweza kuwa na maana kwamba Yesu atakufaau atapaakwenda Mbinguni kwa Baba (m.5, 10, 20 na 21). Na kuwa na maana kwamba Yesu atafufukaau Roho Mtakatifu atakuja. Kisha inaweza kuwa na maana ya kurudi kwa Yesu mara ya pili katika utukufu(m.21-24). Linganisha na 1 Pet 1:5-7 ambapo maneno hayo yametumika pia: Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufufuliwa kwake Yesu Kristo.

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Somabiblia Kila Siku 3

SomaBiblia Kila Siku 3 ni mpango mzuri wa kukusaidia kusoma Biblia kwa njia rahisi. Ufafanuzi wa somo la kila siku unakupa mwanga na kiu ya kuendelea kulitafakari Neno la Mungu ukiwa peke yako au pamoja na wenzako.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana