Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Somabiblia Kila Siku 3Mfano

Somabiblia Kila Siku 3

SIKU 23 YA 31

Musa alikuwa amepata tena mashaka juu ya uwezo wake wa kunena. Na kweli akawa ni Haruni aliyenena kwa Farao si Musa. Alijishuhudia mwenyewe kwamba "mimi ni mtu mwenye midomo isiyo tohara". Lakini Mungu kwa uwezo wake alimfanya Musa kuwa nabii mkuu kati ya manabii wote(Hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso; Kum 34:10). Mungu hutuita jinsi tulivyo, lakini tukijiachia kwa Mungu, yeye anaweza kutufanya kuwa wakuu katika ufalme wake. M.9-13. Hata Shetani anaweza kufanya miujiza, lakini katika kushindana na miujiza ya Mungu hushindwa!

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Somabiblia Kila Siku 3

SomaBiblia Kila Siku 3 ni mpango mzuri wa kukusaidia kusoma Biblia kwa njia rahisi. Ufafanuzi wa somo la kila siku unakupa mwanga na kiu ya kuendelea kulitafakari Neno la Mungu ukiwa peke yako au pamoja na wenzako.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana