Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Somabiblia Kila Siku 3Mfano

Somabiblia Kila Siku 3

SIKU 28 YA 31

Pigo la nne lilikuwa mainzi walioletwa na Bwana kwa wingi sana. Lakini Mungu alitofautisha kati ya Wamisri na Waisraeli. Alitaka kuwatesa Wamisri tu. Mungu aliwalinda watu wake ili hukumu isiwe juu yao(m.20-24). Farao aliwaita Musa na Haruni. Alifikiri kwamba huenda itawezekana kumfanya Mungu apunguze dai lake (m.25). Lakini haiwezekani kumdanganya Mungu au kumfanya Mungu aliye Mtakatifu apunguze madai yake (m.26-29). Ingawa taabu hizi zilikuja juu ya Wamisri, Farao alizidi kuufanya moyo wake kuwa mzito (m.32).

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Somabiblia Kila Siku 3

SomaBiblia Kila Siku 3 ni mpango mzuri wa kukusaidia kusoma Biblia kwa njia rahisi. Ufafanuzi wa somo la kila siku unakupa mwanga na kiu ya kuendelea kulitafakari Neno la Mungu ukiwa peke yako au pamoja na wenzako.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana